Simba yatoa tamko baada ya kuchezea vichapo viwili mfululizo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ambaye ni raia wa Ubelgiji akisaidiana na mzawa, Seleman Matola wamepoteza mechi mbili mfululizo mbele ya timu za majeshi.

Ilianza kuyeyusha pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Nelson Mandela, Oktoba 22 na ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Uhuru, Oktoba 26.


 Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba anaandika namna hii kuhusu mwendo huo:-Salaaam Wanasimba wenzangu!


"Kwanza nitoe pole sana kwa matokeo mabaya mfululizo tuliyoyapata kwenye michezo yetu miwili mfululizo.


"Haya sio mazoea yetu,sio Simba tunayoitaka sisi,lakini ndio ukatili wa huu mchezo ulivyo na kiukweli hatuna budi kukubali yaliyotokea!


"Ndugu zangu najua inauma sana, lakini Simba ni klabu yetu na hatuna klabu nyingine tuipendayo toka moyoni zaidi ya hii.


"Inaweza kufikirisha kidogo Kama tunaweza kurudi katika nguvu yetu, lakini mimi Haji Manara nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kwamba msimu huu hatutachukua ubingwa.


"Muhimu ni kujikosoa pale ambapo labda tunadhani tunateleza na kutorudia makosa ( Kama yapo) Ila mimi narejea kuwaambia inaweza kuwa upepo wa ukatili wa mchezo wenyewe wa mpira,ukizingatia katika mechi zote mbili tulipoteza nafasi kadhaa za kuweza kupata matokeo tofauti na tuliyoyapata!


"Kitu cha kufanya katika kipindi hiki kigumu kwetu ni kuwa na utulivu na kuwa wamoja, namaanisha UMOJA.


"Always (mara zote) Simba ikiwa MOJA huwa haishindwi hivi.


"Na kwa nini nasisitiza hili la UMOJA, hili tumeliandika katika mioyo yetu kama kauli mbiu yetu kuwa Simba Nguvu Moja, tukiliacha, hatujawahi kuwa Simba SC.


"Nimalizie kwa kuwaambia hiki ni kipindi mtacharurwa sana mitandaoni, maofisini na majumbani pamoja na vijiweni kwenu, ichukulieni hyo ndio raha na karaha ya football, isiwasambue hata kama itawaumiza. Naamini soon (karibuni) itageuka kwao, hatujalala ndugu zangu na hatutalala!


"Mimi mitandao yote naona kama imenielemea binafsi lakini nipo strong (imara) na bado imani yangu kuhusu Marathon hii ndefu ni kwamba tunakwenda kuchukua ubingwa wa nne mfululizo. Inshaallah." 


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad