10/06/2020

TFF yatia saini mkataba wa miaka mitatu na Bia ya Serengeti Premium Lager kuidhamini Taifa Stars LEO Oktoba 6 Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) chini ya Rais Wallace Karia, limeingia makubaliano na Bia ya Serengeti Premium Lager na kusaini mkataba wa kuidhamini Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.

 Makubaliano hayo yamefanyika mbele ya Waandishi wa Habari kwenye hafla fupi iliyofanyika Hotel ya Serena ambapo wamezindua pia na jezi za Timu ya Taifa ya Tanzania.


Mkataba huo ni wa miaka miatu wa  kiasi cha shilingi bilioni 3 za Kitanzania.


Kwa sasa timu ya Taifa ya Tanzania ipo kambini ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya FIFA dhidi ya Burundi utakaochezwa Oktoba 11, Uwanja wa Mkapa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger