Ben Pol Atoa Kauli kwa Mashabiki
MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva, Benham Paul ‘Ben Pol’, amewashukuru mashabiki kwa kumpa ushirikiano kila anapotoa nyimbo yake mpya, huku akiwataka waupokee wimbo wake mpya unaoitwa ‘Hiyo Ndo Mbaya’ ambao uko katika staili ya Singeli.

 

Mwanamuziki huyo ameyasema hayo kupitia mtandao wa kijamii.

 

“Nashukuru kwa support ninayopata kutoka kwa mashabiki zangu na wadau, sasa nina miaka 10 kwenye muziki ambapo wamekuwa na mimi bega kwa bega, sasa nimekuja na wimbo wa Singeli unaitwa ‘Hiyo Ndo Mbaya’ ambao nimemshirikisha msanii mpya, Tamimu.

 

“Studio tumefanyia Pizzey Records, Producer ni Jay Stereo, katika kufunga mwaka nitatoa wimbo mpya kila wiki, mashabiki zangu wajiandae kupokea kazi zangu,” alisema na kuongeza:

 

“Pia nimeanza kuzunguka mikoani kufanya matamasha ya kuwashukuru mashabiki zangu; nimeanzia Mbeya, mikoa mingine inafuata naomba wanipokee.”

 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments