11/11/2020

Bonge la EP kamanda, Mfalme wa Young Generation- Dogo JanjaNi 'Updates' kutoka kwa wasanii wa HipHop Bongo Dogo Janja na Young Dee ambao wamekata mzizi wa fitna kwa watu ambao walidhani wana tofauti au bifu kufuatia maneno ambayo yalikuwa yanasemwa kuhusu wao.

Jambo hilo limetokea kwenye mtandao wa Instagram baada ya Dogo Janja kushea 'EP' ya Young Dee huku akimnyooshea mikono juu kwa kumwita mfalme wa wasanii wote wa kizazi hiki cha vijana.


"Kati ya watu niliokutana nao ambao ni Walimu, huyu chalii Youngdaresalama yumo! bonge la EP kamanda, Mfalme wa Young Generation" ameandika Dogo Janja 


Baada ya Post hiyo rapa Young Dee akajibu kwa kuandika kuwa "Young King thanks mwanangu" 


Kwa kauli hizo inaashiria kuwa hakuna tofauti yoyote kati ya wasanii yao na wamemaliza utata wa muda mrefu uliosemeakana kwamba wasanii hao hawana stori wala maelewano mazuri.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger