11/04/2020

Dawa Tisa Mbadala Zinazotibu Ugonjwa wa U.T.I

 


U.T.I ni kifupi cha maneno ya kiingereza: ‘Urinary tract infections’, ni maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo. Ni moja ya ugonjwa unaowakumba sana wanawake kwa sehemu kubwa ingawa hata wanaume pia wanapatwa na ugonjwa huu. Zaidi ya wanawake milioni 8 wanauguwa ugonjwa huu kila mwaka nchini Marekani peke yake.


Kama ulishawahi kupatwa na U.T.I basi hutazisahau dalili zake ambazo mara nyingi huanza kwa hitaji la ghafla la kutaka kwenda kupata haja ndogo na unapofika bafuni mara baada ya kutoa kiasi kidogo cha mkojo utaanza kusikia maumivu kwenye kibofu cha mkojo na hata kwenye urethra. Katika dalili kubwa zaidi utaishia kujisikia homa, baridi kali, maumivu nyuma ya mgongo na hata damu kutoka pamoja na mkojo.

Habari njema ni kuwa kuna dawa mbadala za nyumbani unazoweza kuzitumia na ukajikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu. Endelea kusoma.

Kinachosababisha U.T.I:

 • Kisukari
 • Maumivu ya mishipa
 • Ajari katika uti wa mgongo
 • Ushoga (kwa wanaume)
 • Usafi duni
 • Upungufu wa maji mwilini
 • Kushikilia mkojo muda mrefu
 • Kurithi
 • Kuongezeka ukubwa kwa kibofu cha mkojo au mawe kwenye figo.Baadhi ya dalili za kawaida na zisizo za kawaida za U.T.I

 • Kusikia maumivu wakati wa haja ndogo
 • Kukojoa mara kwa mara
 • Kupatwa ghafla na hitaji la kutaka kukojoa
 • Maumivu kwenye kibofu cha mkojo
 • Mikojo kukutoka pasipo kutaka
 • Hali ya kusikia kuungua wakati wa kukojoa
 • Kukojoa damu
 • Harufu nzito au mbaya ya mkojo
 • Homa
 • Kusikia baridi
 • Kutokujisikia vizuri
 • Kujisikia uchovu
 •  


Dawa mbadala 9 zinazotibu U.T.I
 1. Baking Soda

U.T.I ambayo imedumu zaidi ya siku mbili inahitaji kuripotiwa kwa daktari. U.T.I isiyotibiwa mapema inaweza kuepelekea matatizo zaidi kwenye figo na kuleta matatizo mengine makubwa zaidi. Ili kuzuia U.T.I isijiimarishe zaidi jaribu kuongeza kijiko kimoja cha chai cha baking soda kwenye glasi ya maji na unywe na hivyo kusaidia kupunguza makali au kuendela kwa maambukizi ya U.T.I. Baking soda itapunguza hali ya uasidi katika mkojo wako na kupelekea nafuu haraka. Baking soda ni ile kinamama wanatumia wakati wanapika maandazi. Siri iliyopo hapa ni huko kupunguza asidi kwenye mkojo na mwilini kwa ujumla na hivyo kuongeza hali ya ualikalini mwilini.

  2. Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries):

Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries) ambazo zote zinatoka katika mti wa aina moja na zina sifa sawa ya kudhibiti bakteria. Katika utafiti mmoja, juisi ya zabibu nyeusi iligundulika kuwa na uwezo wa kudhibiti U.T.I. Pendelea kutumia juisi ya matunda haya glasi 2 mpaka 4 kwa siku mara kwa mara ili kujikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu.

 3. Nanasi

Nanasi Kula Nanasi mara kwa mara ni mbinu nzuri kabisa katika kudhibiti maambukizi katika njia ya mkojo. Kwenye nanasi kuna kimeng’enya mhimu sana kijulikanacho kwa kitaalamu kama ‘Bromelain’. Katika utafiti mmoja, watu wenye U.T.I waliopewa hii bromelain sambamba na antibiotic zao walifanikiwa kuondokewa na maambukizi ya U.T.I. Kula vipande vitatu mpaka vitano vya nanasi kila siku kutakuweka mbali na ugonjwa huu.

 4. Maji

maji Kama unasumbuliwa na U.T.I au inakutokea unapatwa na ugonjwa huu mara kwa mara, basi hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku walau glasi 8 mpaka 10 kwa siku, maji yenye joto la kawaida yaani yale ambayo hayajawekwa kwenye friji. Mara nyingi mtu mwenye U.T.I huwa ana upungufu wa maji mwilini na ikiwa utauchunguza mkojo wake utaona ni wa rangi ya njano. Kunywa maji ya kutosha kila siku na kama matokeo yake bakteria wote wanaokupelekea upatwe na U.T.I watalazimishwa kutoka nje ya mwili kupitia mkojo utakaoupata kutokana na kukojoa mara kwa mara kama matokeo ya kunywa maji mengi na utaona baada ya siku 4 mpaka 7 hata rangi ya mkojo inabadilika na kuwa mweupe kabisa. Kujifunza zaidi kuhusu tiba kwa kutumia maji bonyeza hapa.

 5. Vitamini C

Vitamini C husaidia kuzuia uzarishwaji wa bakteria wabaya mwilini
Baadhi ya madaktari wanashauri mtu atumie mpaka mg 5,000 za vitamin C kwa siku kwa mgonjwa anayesumbuliwa na maambukizi ya mara kwa mara kwenye njia ya mkojo. Vitamini C hukifanya kibofu cha mkojo kubaki na afya kutokana na asidi yake safi kwenye mkojo kitendo ambacho ni mhimu katika kuwazuia bakteria wabaya kufanya makazi kwenye kibofu cha mkojo. Ukiacha machungwa, Vitamini C inapatikana pia kwa wingi katika juisi ya ubuyu na kwenye mlonge. Hakikisha unapata kiasi cha kutosha cha Vitamini C kila siku ili kujikinga na hata kujitibu na U.T.I.

 6. Kitunguu swaumu:

Kitunguu swaumu Kitunguu swaumu ni mojawapo ya tiba mbadala ya nguvu katika kutibu maambukizi kwenye njia ya mkojo. Ni dawa nzuri dhidi ya bacteria na virusi na hivyo moja kwa moja kuwa mhimu katika kutibu U.T.I ya jumla na hata ile ya kibofu cha mkojo. Kwakuwa moja ya kazi ya kitunguu swaumu ni kusafisha mkojo basi ni dhahiri inafaa sana katika kutibu U.T.I. Namna ya kukitumia; Chukuwa kitunguu swaumu kimoja na ukigawe mara 2, menya nusu yake (punje 10 au 15), menya punje moja baada ya nyingine na kisha kikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu kisha meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala na mapema uamkapo asubuhi kwa siku 7.

 7. Limau/ndimu:

Limau/Ndimu Weka vijiko vikubwa vitano vya juisi ya limau au ndimu na uongeze maji ili kupata robo lita (ml 250) na unywe kutwa mara tatu. Pia unaweza kuongeza asali vijiko vikubwa vitatu ndani yake. Mchanganyiko huu wa limau na maji ya uvuguvugu utakuondolea maumivu yatokanayo na U.T.I na hata kuzuia kutokwa na damu kama matokeo ya maambukizi ya U.T.I hasa kwenye kibofu cha mkojo.

 8. Unga wa majani ya Mlonge

mlonge Tumia kijiko kimoja cha chakula ndani ya uji,  au ndani ya juisi  ya matunda kikombe kimoja (robo lita) juisi uliyotengeneza mwenyewe, au katika maji ya uvuguvugu kijiko kimoja kikombe kimoja cha maji (robo lita) kutwa mara tatu au unaweza pia kuongeza kijiko kimoja cha unga wa mlonge kwenye mboga ya aina yoyote au katika wali. Tumia kwa mwezi mmoja mpaka mitatu au tumia tu muda wote kama kinga ya mwili wako dhidi ya magonjwa.


9. Mshubiri (Aloe-Vera):

Mshubiri/Aloe Vera Chukua jeli ya mshubiri (aloe-vera) vijiko vikubwa vinne, changanya na maji ya kawaida ili kupata kikombe kimoja (ml 250) au robo lita, changanya vizuri mchanganyiko huu na unywe kutwa mara 2 kwa siku 3 hadi wiki 2 au hadi utakapopona. Unaweza kuongeza asali ndani yake vijiko vikubwa vitatu ili kupunguza ukali wa dawa hii.

Katika dawa hizi zote zilizojadiliwa hapa, napendekeza utumie dawa hizi kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na kwa haraka, nazo ni; maji ya kunywa, kitunguu swaumu, limau, unga wa majani ya mlonge na mshubiri.


Vitu vya kufanya kujikinga usipatwe na U.T.I

 • Ongeza unywaji maji kila siku au juisi za matunda, juisi uliyotengeneza mwenyewe nyumbani.
 • Epuka vinywaji baridi, pombe, chai ya rangi na kahawa.
 • Penda kuwa msafi.
 • Mara zote jitawaze kutoka mbele kurudi nyuma na uepuke kuchangia na wengine vifaa vya bafuni.
 • Pata haja ndogo mara baada ya tendo la ndoa.
 • Usiushikilie mkojo muda mrefu, mara usikiapo kutaka kupata haja ndogo mara moja nenda
 • Vaa nguo za ndani zilizotengenezwa kutokana na pamba.
 • Epuka kaffeina.
 • Epuka tendo la ndoa kinyume na maumbile.
 • Dawa mbadala hizi 9 zinaweza kukusaidia kujikinga usipatwe na U.T.I au kujitibu ingawa bado inashauriwa kwenda kumuona daktari iwapo maumivu au dalili zinadumu kwa muda mrefu.


Kama utahitaji mojawapo ya hizi dawa au kama utakuwa na swali liulize hapo chini kwenye comment Au niachie ujumbe mfupi (sms) kwenye namba 0769142586 au niachie ujumbe WhatsApp +1 805 855 1133.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger