Hatimae Undertaker Ajiuzulu Kucheza MielekaMchezaji maarufu wa mchezo wa mieleka- Undertaker amethibitisha rasmi kujiuzulu kutoka WWE baada ya miaka 30.
Aliingia ulingoni kwa mchezo wa mwisho katika mchezo wa mwisho wa Survivor Series Jumapili usiku, ambapo aliuhutubia umma wa mashabiki wa WWE Universe kwa mara ya mwisho.

Wakati wa hotuba yake , Undertaker ambaye jina lake halisi ni Mark Calaway –alieleza ni kwanini ameamua kujiuzulu.

"Kwa miaka 30 nimekuwa nikiingia ndani ya ulingo huu taratibu na kuwaangusha watu mara kwa mara ," alisema.

"Sasa wangu muda umefika. Muda wangu umefika wa kumuacha My time Undertaker apumzike... kwa ... amani."

Calaway anajiuzuluakiwa ndiye mchezaji bora wa WWE kuwahi kushuhudiwa katika mashindano hayo na amekuwa ulingonikwa miongo mitatu na atakumbukwa na mashapiki wake daima.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments