Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

JPM: RC na DC msiwe na wasiwasi na inawezekana pasitokee mabadiliko yoyote labda atakayefanya mambo ya hovyoRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amewataka watendaji ndani ya serikali kuchaopa kazi na kuachana na wasiwasi wa kuhisi atawaondoa.


Magufuli ameyasema hayo leo Novemba 9, 2020. kwenye hotuba yake baada ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilungi Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilungi akila kiapo mbele ya Rais Magufuli


“Wakuu wa mikoa na wilaya msiwe na wasiwasi na inawezekana pasitokee mabadiliko yoyote labda kwa atakayestaafu au atakayefanya mambo ya hovyo, kama nilikuteua uwezo si bado ni ule ule najua wananisikia wachape kazi wasipochapa kazi shauri yao”, amesema – Magufuli.


“RC unakuwa na wasiwasi gani labda kama ‘performance’ yako ilikuwa haifanyi kazi vizuri, nashangaa napata vimeseji kwamba Mh Rais nimejitahidi katika kipindi changu, kana kwamba kipindi chake nilimwambia kinaisha baada ya mimi kuapishwa”, – ameongeza Rais Magufuli.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments