Steve Nyerere Awapa Onyo kali Billnass na Nandy "Mtakuja kufa misifa yenu"

 


Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kuna picha ambazo zina-trend zikiwaonyesha wapenzi ambao ni Billnass na Nandy wakiwa barabarani wamelala huku wameweka poz la ku-kiss.


Picha hizo zimeleta mjadala kwa mastaa wengine ambao wali-comment kwenye post hiyo akiwemo msanii wa filamu Steve Nyerere ambaye amewaonya kwamba wasilete mapenzi barabarani kwani watakuja kufa.


"Mtakuja kufa misifa yenu hiyo haya, jifanyeni kama nyie ndiyo wa kwanza kupendana, watu wanajua mapenzi toka 1981 lakini hawajawahi kucheza na barabara, sisi tunataka kusikia shemeji kaingia leba, hayo mnayofanya hata sisi kwenye sinema tunafanyaga nyau nyie" ameandika Steve Nyerere 


"Mapenzi yenu yanaweza kuwa yamoto ila sio ya moto kama hiyo barabara ndugu zangu" Comment ya Idris Sultan 


"Kuna saa natamani ningekuwa mimi ndiyo hiyo lami" Dj Choka 


"Ooooh, mkijagongwa na gari hapo hasara kwa nani, halafu mbona kama Billnass hauna furaha kwani umelazimishwa kwenda" Roma Mkatoliki

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments