Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Tanzania Yanyakua Ubingwa wa COSAFAWU17

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURETIMU  ya Wanawake Chini ya Umri wa Miaka 17 #Under17 ya Tanzania imeibuka mshindi wa mashindano ya #Cosafa 2020 baada ya kuifunga  Zambia kwa mikwaju ya penati 4-3 katika Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini, mchana huu baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90.
Zambia ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la mapema kunako kipindi cha kwanza dakika ya 18 kupitia kwa Comfort Selemani ambalo lilidumu mpaka kipindi cha pili dakika ya 90.
Mwamuzi aliongeza dakika tano kufidia muda uliopotea katika matukio mbalimbali ambapo dakika ya 90+4′ Tanzania ilipata penati baada ya mchezaji wake kufanyiwa madhambi ndani ya penati boksi. Tanzania ilifanikiwa kusawazisha kupitia penati hiyo iliyopigwa na Koku Kipanga mpaka mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho, Tanzania 1-1 Zambia.
Miamba hao walitengewa matuta ambapo Tanzania aliibuka na ushindi wa penati 4-3 na kutawazwa kuwa mabingwa wa COSAFA Women Championship. Tanzania imeingia kama timu mwalikwa katika michuano hiyo.

Post a Comment

0 Comments