Wachezaji Simba Wala Kiapo Nigeria
KIKOSI cha Simba, juzi Jumatano kiliwasili jijini Abuja nchini Nigeria tayari kuwavaa wenyeji wao, Plateau United ya nchini humo katika mechi ya kwanza ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Jumapili hii, Simba inatarajiwa kuvaana na Plateau United, kisha timu hizo kurudiana kati ya Desemba 4-6, mwaka huu jijini Dar kusaka nafasi ya kuingia hatua ya kwanza ya michuano hiyo mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Katibu wa Simba, Arnold Kashembe, amesema kikosi cha wachezaji 24 kilisafiri salama kutoka jijini Dar hadi Ethiopia ambapo kilipumzika kwa muda kisha juzi asubuhi kulekea Nigeria.

 

“Maandalizi ya mechi yetu dhidi ya Plateau yalishakamilika tangu kikosi kilipokuwa hapa, mwalimu ameandaa mikakati yake ya ushindi kuhakikisha tunafanikiwa kupata pointi tatu ugenini.

 

“Kikosi kilitua Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kuunganisha ndege ambapo kililala pale na asubuhi kilielekea Nigeria kikiwa salama na kufika mchana wake w, maandalizi yapo vizuri kwa upande wa uongozi kuhakikisha timu inarudi na ushindi,” alisema Kashembe.

 

WACHEZAJI WALA KIAPO

Kuelekea katika mchezo huo, wachezaji wa Simba wamekula kiapo cha kuibuka na ushindi wakiwa ugenini.

Erasto Nyoni ambaye ni beki wa kikosi hicho, alisema: “Tunahitaji kufika mbali katika michuano hii, tunakumbuka ilivyotokea msimu uliopita, hivyo hatupo tayari kuona jambo hili linatutokea tena, msimu huu tunahitaji kupambana zaidi na ushindi ndio malengo yetu.”

 

Naye beki mwingine wa kati wa kikosi hicho, Ibrahim Ame, alisema kuibuka na ushindi ugenini itakuwa ishara nzuri kwao katika michuano hii ya kimataifa.

“Ugenini katika mpira huwa kuna maana nyingi sana, hatutaki kupoteza mchezo wetu, sidhani pia kama kuna mwana Simba atafurahi kuona timu imepoteza, sisi kama wachezaji tutahakikisha tunapambana ili kupata ushindi tukiwa ugenini ambao utakuwa na faida kubwa sana kwetu,” alisema mcheza huyo.

 

BOCCO JEURI TUPU

Mshambuliaji na Nahodha wa Simba, John Bocco, amesema wamesahau matokeo yao yaliyopita kwenye ligi waliposhinda 7-0 dhidi ya Coastal Union, na sasa akili zake amezielekeza kwenye mchezo wao huo dhidi ya Plateau United

 “Msimu uliopita timu yetu ilifanya vibaya katika michuano hii baada ya kutolewa katika hatua ya awali dhidi ya UD Songo, hivyo msimu huu hatutaki ijirudie tena.

“Tunafahamu msimu uliopita mashabiki walichukizwa kutolewa mapema, hivyo safari hii tumefanya maandalizi mazuri yaliyokwenda na usajili bora, imani yetu ni kufanya


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments