Wamejitoa Kimasomaso, Mungu Amewaona
WAHENGA walisema kuwa na mtoto siyo nguo useme utamuomba mtu! Ndivyo ilivyokuwa kwa baadhi ya mastaa Bongo ambao waliamua kujitoa kimasomaso ndani ya mwaka huu wa 2020 unaoelekea ukingoni. Wengine wamejikuta Mungu akiwaona na kuwabariki kupata watoto na wengine wakinasa mimba.

 

Wengine wameshajifungua na sasa wanalea watoto wao. Miaka kadhaa nyuma, mastaa wengi walikuwa wana­ cha watoto wao kukwepa kuonekana wamezaa mapema au wamama hivyo wakati mwingine kuwaita watoto waliowazaa ni wadogo zao, jambo ambalo kwa sasa ni tofauti kabisa. Wafuatao ni baadhi ya mastaa wa kike Bongo waliopata watoto ndani ya mwaka huu wa 2020 na wengine wanatarajia kujifungua;

 

KIDOA SALUM

Huyu ni pisi kali aliyepata umaarufu kupitia kuuza sura kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva. Baada ya hapo alianza kukiwasha kwenye Bongo Movies na anaonekana sawia kwenye Tamthiliya ya Huba. Kidoa amejaaliwa kupata mtoto wa kike aitwaye Kish na bado anaonekana mrembo wa nguvu.

 

MWANAHERI

Huyu ni zao la Bongo Movies ambaye alianza kuwika miaka minne iliyopita. Aliingia kwenye ndoa miaka miwili iliyopita na sasa amebahatika kupata mtoto hivi karibuni aliyempa jina la Fatuma ‘Fetty’. Mwanaheri alikuwa ak‑ ipenda mno hivyo hata baada ya kujifungua, bado anaonekana mrembo na anayejipenda kama zamani ak‑ iita jina la Mama Tuma.

 

ROSE NDAUKA

Ukitaja listi ya waigizaji bora kabisa wa Bongo Movies, huwezi kuacha kutaja jina la Rose Ndauka. Rose alianza kuwika kitambo, lakini naye mwezi mmoja iliyopita alibahatika kupata mtoto wa kiume.

 

Hata hivyo, huyu ni mwanaye wa pili baada ya yule wa kwanza wa kike aliyempata kwenye ndoa yake ya kwanza na sasa yupo kwenye ndoa yake ya pili. Pamoja na kuwa na mtoto mwanzoni, lakini baada ya kujifungua huyu wa pili, anaonekana kuwa na furaha mno ya kuitwa mama kwa mara nyingine.

 

AUNT EZEKIEL

Wengi sasa hivi wanapenda kumuita Mama Cookie. Huko nyuma kuna walio­ kiri suala la kuzaa kwake litakuwa ni changamoto, lakini siyo kweli. Ni mwigizaji ambaye al‑ ivunia kuwa mjamzito tangu siku ya kwanza alipogundua amebeba mimba yake ya kwanza.

 

Kwa sasa yupo huru na ujauzito wake wa pili na ndiyo maana muda mwingine anauachia wazi unaonekana. Aunt amekuwa akieleza ni kwa kiasi gani anapenda watoto na yupo tayari kuzaa hadi pale atakapoambiwa na madaktari kuwa sasa inatosha. Kwa sasa amepachikwa jina la Mama K na anatarajia kujifungua wakati wowote.

 

POSHY QUEEN

Huyu ni mrembo maarufu mtandaoni (sosholaiti). Jina lake halisi ni Jacqueline Obeid. Baadhi ya watu waliamini kuwa hawezi kubeba mimba kirahisi kwani ataho­fia kupoteza ile shepu yake, lakini cha ajabu amewashangaza kwa kubeba mimba na kujifungua bila kujali kwamba atapoteza urembo wake. Ukweli ni kwamba naye anajivunia kuitwa mama kwa kipindi hiki ambacho ni mchumba wa mtu akisubiri kufunga ndoa na kuangusha shughuli ya kukata na shoka.

 

JACQUELINE WOLPER

Muigizaji huyu wa Bongo Movies amekuwa tofauti kabisa na wengine. Mimba yake imekuwa ni siri kubwa kwani ameamua kujiweka ‘karantini’ ili watu wasione kitumbo chake.

 

Hata hivyo, anakiri kwamba mwaka huu wa 2020, umekuwa ni mwaka wake wa furaha baada ya kunasa ujauzito ambao amekuwa akiutafuta kwa muda mrefu kutokana na kupewa majina mabaya yaliyotokana na umri kusogea bila kupata mtoto.

Inafahamika kwamba, Wolper kwa sasa yuko kweye uhusiano wa kimapenzi na mfanyabiashara wa nguo j‑ ini Dar, Rich Mitindo na ndiyo mwenye kitumbo hicho.

Makala: Imelda Mtema, Bongo

 

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments