Bondia Mrembo Mbaroni Kwa Kumuua MumeweBONDIA mwanamama wa ngumi za kulipwa nchini Brazil ambaye alipigania mara tatu ubingwa wa dunia, Vviane Obenauf anashikiliwa na Jeshi la Polisi la nchini Sweden kwa tuhuma za kumuua mume wake.

 

Viviane ambaye ni mzaliwa wa Brazil mwenye umri wa miaka 34, anatuhumiwa kumpiga mumewe tajiri anayefahamika kwa jina la Thomas raia wa Uswisi hadi kufa katika mgahawa wake huko Sweden.Kulingana na taarifa kutoka Sports Boxing na Boxing Scene zinasema, bondia huyo alikamatwa mapema na maofisa polisi ambao wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kama kweli alihusika na majeraha yaliyokutwa kwenye mwili wa mumewe huyo.

 

Viviane anatajwa kuwa moja kati ya mabondia wakorofi nje ya ulingo kwani hii siyo mara ya kwanza yeye kuhusika na vurugu, pia alishawahi kumchapa mchumba wake wa zamani huko London, England baada ya kumzingua kwenye sherehe za siku yake ya kuzaliwa.
 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments