"Christian Bella amenifanyia figisu" - Jacky Chant

 

Jacky Chant ni jina lililosikika likitajwa na Christian Bella kwenye nyimbo ya 'nakuhitaji' na 'amerudi' kutoka bendi ya Malaika, ila kwa sasa kuna ugomvi kati ya wasanii hao hali iliyopelekea Jacky Chant kujitoa kwenye bendi hiyo.


eNewz imepiga stori na Jacky Chant mwenyewe kuhusu chanzo cha ugomvi wao ambapo amesema alifanyiwa figisu kwamba uwezo wake unaweza ukamzidi Christian Bella ndiyo maana akatolewa.


"Kilichosababisha mimi kuondoka haikuwa pesa bali ni wapambe wa jamaa walikuwa wanamjaza kwamba akiniachia mimi nitakuja kupanda zaidi na kumpita yeye , niliona figisu zimezidi hivyo nikaondoka, kila mtu ana wakati wake na huu ndiyo wakati wangu, wakati wa Christian Bella na Nyoshi umeshapita" ameeleza Jacky Chant

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments