Facebook Yakabiliwa na Kesi ya Kutaka Kuua Kampuni Pinzani

 


Kampuni ya #Facebook Inc inaweza kulazimishwa kuuza mali zake ikiwemo #WhatsApp na #Instagram baada ya Tume ya Biashara ya #Marekani kufungua mashtaka dhidi ya kampuni hiyo ikisema ilitumia mkakati wa "kununua au kuzika" kuwarubuni washindani wake


Facebook inakuwa kampuni ya pili kubwa kwenye Uwanja wa #Teknolojia kukabiliwa na changamoto ya kisheria mwaka huu baada ya Idara ya Sheria ya Marekani kuishtaki Google Alphabet Inc mnamo Oktoba, ikiishutumu kutumia nguvu katika soko ili kujilinda na wapinzani


Kesi hiyo iliyofunguliwa Jumatano inaishutumu Facebook kwa kuwanunua wapinzani, ikiwemo Programu ya Picha (Instagram) kwa Dola bilioni 1 mwaka 2012 na Programu ya Ujumbe (WhatsApp) kwa Dola nilioni 19 mwaka 2014.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments