Kijana ahukumiwa miaka 30 jela kwa ubakaji

Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kijana aliyefahamika kwa jina la Halawa Tabu mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti mwenye umri wa miaka 19.
Awali katika Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora, Wakili wa Jamhuri, Miraji Kajiru aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo la ubakaji mwezi Julai mwaka huu Kinyume na Kifungu cha 130 kidogo cha kwanza na cha pili (a) na kifungu cha 131 kidogo cha kwanza sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Julai 19 aliitwa nyumbani kwa binti aliyembaka na baba mzazi wa binti huyo kwa lengo la kuzindika nyumba yao ndipo ilipofika usiku kijana huyo Tabu akaomba amchukue binti huyo ambaye jina linahifadhi kwenda naye porini ili akamuoshe dawa za kuondoa mikosi mwilini na akafanikiwa kufanya tukio hilo alilokusudia.

Shauri hilo la ubakaji namba 66 la mwaka 2020 upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi saba huku upande wa mshtakiwa Halawa Tabu alikuwa akijisimamia mwenyewe.

Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora Jocktan Rushwela baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili alijiridhisha pasipo shaka yoyote ndipo akamuhukumu adhabu yenye ukomo kutumikia kifungo cha miaka 30 jela.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments