Kocha Zidane Akalia Kuti Kavu Real Madrid, Wampe Mechi Hizi la Sivyo Out

 


Imeelezwa kuwa baada ya matokeo mabovu ya hivi karibuni, kocha wa Real Madrid, #ZinedineZidane amepewa mechi nne zitakazoamua mustakabali wake ndani ya klabu hiyo.


Katika msimamo wa kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya, #Madrid inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi saba, ambazo sawa na Shaktar Donetsk anayeshika nafasi ya tatu, Borrusia Monchegladbach anaongoza kundi hilo kwa pointi nane na Inter Milan anaburuza mkia kwa pointi tano.


Kwa mujibu wa mtandao wa Marca wa nchini Hispania, mtihani huo wa #Zidane utaanza katika mchezo wa Jumamosi hii ambao ni wa Ligi nchini humo maarufu La Liga dhidi ya Sevilla, kabla ya wiki ijayo kukutana na Monchegladbach katika mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa utakaopigwa Uwanja wa Bernabeu.


Michezo mingine ni dhidi ya Atletico Madrid na Athletic Club yote ya La Liga.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments