Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kumekucha Bongo Muvi, Msanii Arudi Bongo Tuzo ya Kimataifa
Wasanii wa Bongo Muvi baada ya kumpokea mwenzao Shaykaa (watatu kushoto).

Kumekucha Bongo Muvi hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia wasanii wa tasnia hiyo jana jioni kufurika Uwanja wa Julius Nyerere kumpokea mwenzao, Shahista Alidina ‘Shaykaa’ baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere akitokea Dubai kupokea tuzo ya kimataifa ya Word Oscars Signature Award katika kipengere cha muigizaji bora wa kike kutoka Tanzania.


Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Filamu Tanzania, Emmanuel Ndumukwa akiibusu tuzo hiyo baada ya kumpokea Shaykaa (kulia).

Mwishoni mwa wiki iliyopita Bodi ya Filamu nchini kupitia Kaimu Katibu Mtendaji wake, Dk. Kiango Kilonzo ilimtangaza msanii huyo mbele ya wanahabari kuwa ameshinda tuzo hiyo nchini humo na kumkabidhi bendera kwa ajili ya kwenda kuipokea.


Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania (TDFAA), Chiki Mchome akizungumza kwenye mapokezi hayo.

Dk Kilonzo alisema Shaykaa alishinda tuzo hiyo kupitia filamu iitwayo Uhuru na gharama zake akicheza kama mwenye ugonjwa wa akili ndipo nafasi hiyo ikamtoa na tuzo hiyo ya kimataifa katika tuzo za Word Oscars Signature Award.


Msanii Mike Sangu akimpongeza Shaykaa baada ya mapokezi hayo.

Shaykaa baada ya kutua uwanjani hapo ilikuwa ni nderemo kwa wasanii wa Bongo Muvi ambapo msanii huyu alianza kwa kuwashukuru wenzake hao kwa sapoti yao tangu siku alipotangazwa mshindi wa tuzo hiyo, Desemba 18 mwaka huu.


Piga kelele kwa tuzo akeee…. weeeweeeee…. Msanii Natasha akipozi na tuzo hiyo.

Mapokezi hayo yaliongozwa na maofisa wa Bodi ya Filamu akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Filamu, Emmanuel Ndumukwa aliyewaongoza maofisa wenzake wa bodi hiyo.

Afisa huyo baada ya kumpokea msanii huyo alimpongeza kwa juhudi zake kwa kuipatia heshima kubwa tasnia hiyo na nchi kwa ujumla.


Mzee Chilo akiichum tuzo hiyo na kisha ndipo akaanza kutoa maneno ya hekima wakati akimpongeza Shaykaa aliyekuwa akizungumza na Global Tv (kulia).

Afisa huyo aliwapongeza na wasanii waliofika kumpokea mwenzao kwa kitendo chao cha kuonesha kumpa sapoti jambo linalochagiza maendeleo kwenye tasnia hiyo, Afisa huyo wa Bodi ya Filamu.

Upande wa Bongo kulikuwa na kundi kubwa la wasanii akiwemo Chiki Mchome, Mike Sangu, Suzan Lewis ‘Natasha’ Yvone Cherry ‘Monalisa’ Ahmed Ulotu ‘Mzee Chillo’, Pierre Pierre na wengineo ambao nao walimpongeza mwenzao kwa ushindi huo wa kimataifa na kusema ushindi huo ni wao wote na umewafungulia mlango na wao kunyemelea tuzo zingine kama hizo.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments