Messi "'Kushindwa Kuondoka Barcelona Kumeniathiri Msimu Huu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Lionel Messi amesema jaribio lake la kutaka kuondoka Barcelona ambalo liligonga mwamba katika dirisha la uhamisho lililopita liliathiri sana mchezo wake msimu.

Mwezi Agosti mwaka huu mshambuliaji huyo njota wa Argentina alisema anataka kutumia kifungu cha sheria katika mkataba wake ambacho kingemwezesha kuondoka katika klabu hiyo.


Lakini Barcelona ilikataa, ikisema kuwa malipo ya ada ya Yuro milioni 700(£624m) lazima yaafikiwe.


"Nilivuta kila kitu hadi mwanzo wa msimu," Messi, 33, aliambia kituo cha televisheni cha Kihispania cha La Sexta.


"Ukweli ni kwamba sasa sina neno, lakini dirisha la uhamisho lililopita ulikuwa wakati mbaya sana."


Messi alifikia rekodi ya mchezaji mkongwe wa Brazil Pele ya kufunga magoli 643 ndani ya klabu kwa kuisawazishia Barcelona bao lililoiwezesha kutoka sare dhidi ya Valencia siku ya Jumamosi.


Lilikuwa bao la tisa katika mechi 17 za Barcelona, ambao wako nafasi ya tano katika La Liga.


Messi, ambaye anaweza kuondoka Barcelona bila malipo mkataba wake utakapokamilika mwisho wa msimu huu, anaweza kujadiliana na klabu nyingine kuanzia Januari mosi.


Rais wa mpito wa Barcelona Carlos Tusquets, ambaye alichukuwa nafasi ya uongozi wa klabu hiyo hadi uchaguzi utakapofanywa mwezi Januari baada ya Josep Maria Bartomeu kujiuzulu Oktoba, amesema "kulingana na tathmini ya kifedha " Messi angekuwa ameuzwa katika dirisha la uhamisho lililopita .


Wachezaji wa Barcelona walikubali kupunguziwa marupurupu mwezi Novemba ili kuwawezesha washindi hao mara 26 wa taji la La Liga kuokoa Yuro milioni 122(£110m).


"Kwa sasa najihisi vyema na natarajia kukabiliana vilivyo kushinda katika kila shindano lililopo mebele yetu," alisema Messi.


"Nafahamu klabu inakabiliwa na hali ngumu kwa sasa katika ngazi ya usimamizi, uwanjani na kila kitu kinachozunguka Barca kwa sasa ni kigumu , lakini najihisi mwenye furaha''.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad