Mstaafu Mwinyi Ampa Tano Magufuli


Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Dkt. Ali Hassan Mwinyi ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli kwa kulivusha Taifa la Tanzania salama katika nyanja mbalimbali ikiwemo ukuaji wa uchumi pamoja na mapambano dhidi ya gonjwa la Korona

Dkt. Ali Hassan Mwinyi ametoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya tatu ya Chuo cha Kampala University (KIUT) ambapo amesema serikali ya awamu ya tano imepiga hatua kubwa ya maendeleo katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi.Aidha Dkt. Mwinyi ambae ni Mkuu wa chuo hicho cha (KIUT) amesisitiza kwamba Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa kielelezo cha kweli cha namna ambavyo mtu aliyeelimika anapaswa kufikiri na kutenda.


  Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Dkt. Ali Hassan Mwinyi akimpongeza mmoja wa wahitimu wa Chuo hiko.


“Mheshimiwa Rais ametuonesha na kutukumbusha jinsi ambavyo msomi anapaswa kushiriki kikamilifu katika kuisadia jamii kutatua changamoto inazokabiliana nazo” amesema Dkt. Ali Hassan Mwinyi.


Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Tanzania (KIUT) Dkt. Mouhamad Mpezamihigo, ametoa wito kwa watanzania wote kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa viongozi mbalimbali ili kushiriki katika ujenzi wa nchi kupitia utoaji wa elimu ya juu bora kwa wananchi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments