Rais Anataka Kuunganishwa Kwenye Magroup ya WhatsApp

 


Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, ameweka namba yake ya simu mtandaoni kupitia akaunti yake ya Twitter, na kusema “Nialikeni kwenye vikundi vyenu.”.

Maduro alirekodi video na kutoa ujumbe uliosema, “Venezuela, ninashiriki katika vita vya maoni kwenye vikundi vya WhatsApp na Telegram kwa nambari 04262168871, nijumuisheni kwenye vikundi vyenu vyote na tupambane pamoja kutetea Venezuela,”.

Katika nambari hiyo aliyoitoa, ilionekana kuwa na picha yake Rais Maduro iliyobeba maneno yanayosoma “Rais wa Venezuela” kwenye profile ya WhatsApp na Telegram.

Maduro pia alichapisha video za ujumbe aliotumiwa kwake kupitia akaunti kituo rasmi cha Telegram.

Maduro alimalizia kusema, “Mapokezi yamekuwa makubwa sana, maelfu ya vikundi vimenijumuisha,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

1 Comments

  1. Huyu Maduro ni Jembe alilo liwacha Hugo Chaves.
    Anawekewa Mizengwe na Mataifa makubwa.. Lakini Kidume anachapa Kazi kwenda mbele kama JPJM.

    Wamejaribu vibaraka wakazi ndani na nje Maandamano / Kumpindua kwa kutumia Mamluki walio ingia kwa njia ya Bahari

    Yote yamegonga Mwamba. Kisa Nchi Tajiri. Mabeberu wana Tamaa

    ReplyDelete