Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Simba: Tutashinda kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinun

 


SHOMARI Kapombe, beki wa kulia wa Klabu ya Simba amesema kuwa wanaamini watashinda kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinun utakaochezwa kesho, Desemba 23 Uwanja wa taifa wa Zimbabwe.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji akisaidiana na Seleman Matola ambaye ni mzawa itamenyana na FC Platinum kwenye mchezo wa raundi ya kwanza hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


 Kapombe amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanya kwenye mchezo wao ila wanaamini watafanikiwa kwa kuwa wamekubaliana kupambana.


“Wachezaji kwa ujumla tumekubaliana kufanya kazi kwa juhudi kuweza kupata matokeo kwani hakuna kitu kingine ambacho tunakihitaji zaidi ya ushindi ndani ya uwanja.


“Tutakuwa ugenini ila haimaanishi kwamba tutakuwa wageni uwanjani hapana. Hatutakuwa wanyonge tutapambana kwa nguvu kupata matokeo,” amesema Kapombe. 


Simba imetinga hatua hii ya kwanza baada ya kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Plateau FC ya Nigeria mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa New Jos Nigeria.


Mchezo wa pili Uwanja wa Mkapa, Simba iliweza kulinda ushindi wake na kufanya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana.


Mechi zote mbili Kapombe alikuwa ni chaguo la kwanza la Sven ndani ya uwanja.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments