Watu 16 wapoteza maisha baada ya basi la abiria kushambuliwa

 


Watu 16 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya basi la abiria kushambuliwa katika jimbo la Kano nchini Nigeria.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya kitaifa, watu wasiojulikana walishambulia basi la abiria katika eneo la Dambatta lililoko kwenye barabara kuu inayounganisha mji mkuu wa Abuja na Kano.


Watu 16 walipoteza maisha kwenye uvamizi huo na wengine wengi walijeruhiwa.


Gavana wa jimbo la Kano Abdullah Umar Ganduje, amelaani uvamizi huo na kusema kuwa vikosi vya usalama vilitumwa kwenye eneo la tukio na kuanzisha uchunguzi.


Eneo hilo limekuwa likikumbwa na mapigano makali kati ya jamii ya Fulani ambao ni wafugaji na makabila mengine yanayojishughulisha na kilimo.

That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments