WHO: Mzozo wa Covid-19 Hauna Mwisho


Mwenyekiti wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO ) Tedros Adhanom Ghebreyesus, ameonya kuwa mlipuko janga la corona (Covid-19) hautakuwa mwisho wa mizozo.

Tedros, alitoa ujumbe kupitia video katika Siku ya Maandalizi ya Janga la Kimataifa na kusema,


"Historia inatuambia kuwa hili sio janga la mwisho na kwamba magonjwa ya kuambukizwa ni hali ya kawaida ya katika maisha,"


Mwenyekiti huyo huyo wa WHO alisema kuwa uwekezaji bora katika afya ya umma, unaoungwa mkono na serikali na jamii, ‘‘utawezesha vizazi vya sasa na vijavyo kurithi ulimwengu wenye usalama, uthabiti na ulio endelevu zaidi."


Akibainisha kwamba janga la corona "limegeuza ulimwengu" wa kijamii na kiuchumi katika miezi kumi na mbili iliyopita, Tedros, alisisitiza kuwa janga hilo sio "kushangaza", kwa kuwa wametoa onyo mara nyingi kwa miaka mingi juu ya kutokuwa tayari kwa ulimwengu.


Mwenyekiti wa WHO pia aliongezea kusema,"Tunahitaji kujifunza vizuri sana kwa janga hili," na funzo hili halijumuishi tu sekta ya afya, bali pia uwekezaji katika uwezo wa utayari wa serikali nzima na jamii kwa ujumla.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments