1/24/2021

Alikiba Afunguka Baba Diamond ni ‘Baba Yangu’
MAMBO ni mengi muda mchache! Wakati sakata la baba halisi wa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ likiendelea kujadiliwa mitandaoni, mapya yameibuka kwa upande mwingine, Gazeti la IJUMAA lina mchapo kamili. Imefahamika kwamba, Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ ni mtu wa karibu wa mzee Abdul Juma ambaye amezua sekeseke la kuambiwa si baba halisi wa Diamond au Mondi.

 

⚫️ Kwa UPDATES za NAFASI ZA KAZI, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

 

MAONI YA WENGI

Baada ya sakata hilo lililoibuliwa na mama yake, Diamond au Mondi, Sanura Kassim ‘Sandra’ kutikisa, maoni ya wengi yalionekana kumuona huruma Mzee Abdul kwani amejinasibu kama mzazi wa Mondi kwa muda mrefu.

 

Watu mitandaoni walisema, kitendo cha mama Mondi kuanika jambo hilo hadharani kwenye chombo cha habari, hakikuwa cha kiungwana na kwamba alipaswa kulimaliza suala hilo ki-utu uzima.“

 

Kitanda hakizai haramu, hata kama ni kweli hakuwa mwanaye, lakini amemlea, ana sababu gani ya kutangaza sasa hivi kuwa si mzazi wake?” Alihoji mdau mmoja mtandaoni.KIBA, HARMO WATAJWA

Kwenye jambo hilo, wasanii ambao wanaonekana kuwa na usindani na Mondi wakiwemo King Kiba na Rajabu Abdul ‘Harmonize’ walitakiwa kujitokeza angalau kumfariji anayemheshimu kama baba yake na anamshukuru kwa sapoti yake kubwa.

 

Staa huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya wa Infidele alizidi kusisitiza kuwa, mzee huyo amekuwa kama mzazi wake kwa kipindi kirefu hivyo anamjua kama mwanaye.

 

⚫️ Kwa UPDATES za NAFASI ZA KAZI, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

 

“Kitu ambacho watu wengi hawakijui ni kwamba Mzee Abdul ananijua mimi tangu nikiwa mdogo, kipindi hicho tunaishi wote Kariakoo (Dar) hivyo ananichukulia kama mwanaye, binafsi ninaheshimu sana,” alisema Kiba.

 

KUHUSU KIPANDE CHA VIDEO…

Alipoelezwa kuhusu kipande cha video kinachomwonesha Mzee Abdul akiimba wimbo wake huo mpya na kusindikiza na kutamka ujumbe wa kumtakia heri, Kiba alisema; “Alichokizungumza kwa sababu huwenda wimbo wangu umegusa mno maisha yake kwa kiasi fulani.”

 

ILIKUWA HIVI…

Awali, Mzee Adul alionekana kwenye video akisikiliza wimbo mpya wa Kiba wa Infidele na kama si kumsaidia Mzee Abdul.Maoni mengi yalionesha yalitawala mitandaoni kuwa, kama Mondi amekuwa kimya baada ya mama yake kutamka hivyo, maana yake anamuunga mkono hivyo Mzee Abdul anapaswa kusaidiwa.“Kiba na Harmo, jitokezeni mumsaidie huyu mwenzenu pengine hatambui thamani ya mzazi,” alichangia mdau mwingine huko Instagram.

 

KIBA, HARMO WATAFUTWA

 

Kufuatia maoni mengi ya mtandaoni na wengine kupiga simu chumba cha habari, Gazeti la IJUMAA liliona si vibaya liwatafute Kiba na Harmo ili kuwasikia wanazungumziaje suala hilo.HARMO ATAFUTWA Wa kwanza kutafutwa alikuwa ni Harmo, lakini bahati mbaya simu yake iliita bila kupokelewa na ndipo zoezi hilo lilipohamia kwa Kiba.

 

ASEMA WANAFAHAMIANA KITAMBO

Kiba alisema Mzee Abdul ni mzee kusema;“Ali Kiba ndugu yangu, mwanangu, swahiba wangu, rafiki yangu nimeupenda wimbo wako, nina imani itatoa fundisho, imeniguza sana tena nafsi yangu. “Endelea…Mwenyezi Mungu akupe power, akutolee nuksi na balaa, muziki wako uendelee kama muziki wako, kaza buti, achana na Mswahili. Mungu ndiye peke yake anabakia Mungu, endelea na muziki wengine wote usiwasikilize.

 

Ali Kiba Mungu akubariki.”

TUJIKUMBUSHE

Wiki iliyopita, Mama Dangote alikinukisha kwenye mitandao baada ya kunukuliwa akisema baba halisi wa mwanaye Diamond ni marehemu Salum Idd Nyange.Alisema, ukweli wa suala hilo ambalo lilikuwa siri kwa watu wengi ndiyo huo alioutamka na kwamba Mzee Abdul ni baba mlezi wa Mondi kwa maana kwamba alishiriki kwa kiasi fulani katika malezi.Kwa zaidi ya miaka 30 sasa, Mondi alikuwa akitumia jina la Nasibu Abdul Juma hivyo jambo hilo limesababisha watu wengi kupigwa na butwaa!

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger