Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Babu wa Miaka 80 Akutwa Amekufa Guest Mbezi Beach Akiwa na Mpenzi Wake

Mwanaume aliyejulikana kwa jina la David Makerege Mluli (80) amekutwa amefariki dunia ndani ya Hoteli ya Mbezi Garden iliyopo Mbezi jijini Dar es salaam akiwa na mpenzi wake aliyejitambulisha kwa jina la Neema Kibaya (33).


Download App ya Udaku Special HAPA Kusoma Hizi Habari Kupitia Simu yako KirahisiKamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni ACP Ramadhan Kingai amesema tukio hilo limetokea Januari 16,2021 majira ya saa 9 alasiri katika eneo la Mbezi Beach ambapo Jeshi la polisi lilipokea taarifa kutoka kwa Meneja wa Hoteli ya Mbezi Beach Garden, Newton Mkonda kuwa katika hoteli hiyo kuna mteja amefariki dunia.

"Baada ya taarifa hiyo kupokelewa, Jeshi la polisi lilifika katika hoteli hiyo chumba namba 22 na kubaini uwepo wa maiti ya mwanaume ambaye baada ya kupekua katika nguo zake vilikutwa vitambulisho vyenye majina ya David Makerege Mluli (80) mkazi wa Goba aliyekuwa amekodi chumba hicho",ameeleza


"Pia katika chumba hicho alikutwa mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Neema Kibaya (33) mkazi wa Goba ambaye katika maelezo yake alieleza kuwa marehemu alikuwa mpenzi wake", ameongeza Kamanda Kingai.

Kamanda Kingai amesema uchunguzi wa awali ulifanyika na kubaini kuwa mwili wa marehemu hauna jeraha lolote na kuchukuliwa na askari polisi kupelekwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi na hifadhi.


Download App ya Udaku Special HAPA Kusoma Hizi Habari Kupitia Simu yako KirahisiAidha amesema mwanamke huyo aliyekutwa chumbani ambamo mwili wa marehemu ulikuwemo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments