Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mastaa Hawa Bye Bye 2020…. Kicheko 2021

DAR: Wakati leo tukifungua pazia la Mwaka Mpya wa 2021, mikakati na malengo yaliyowekwa na Serikali na watu wa kada mbalimbali yameashiria kicheko katika mwaka huu ambao unaelezwa utafuta machungu ya mwaka jana, Gazeti la IJUMAA linachambua.

 

Hatua hiyo inatokana na ukweli kuwa mwaka 2020, ulikuwa mwaka wa kutetea uhai zaidi kitu chochote kutokana na madhara makubwa ya janga la Virusi vya Corona ambavyo vimechukua uhai wa watu milioni 1.8 duniani.

 

Corona ilisababisha kila sekta kusimama na kulazimisha watu kujifungia ndani ilihali kwa upande wa Tanzania kulikuwa na ahueni kutokana na mkono wa Mungu na ujasiri wa Rais Dk John Pombe Magufuli.

 

Athari za Corona, zimedhihirika kwenye sekta ya sanaa, elimu, utalii, afya na huduma nyingine muhimu ambazo zimedumaza ukuaji wa pato la mtu mmojammoja na Taifa kwa jumla.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments