Mchungaji wa Kenya ahukumiwa miaka 140 baada ya kuwabaka binti zake wawili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Mahakama nchini Kenya imemfunga kigfungo cha miaka 140 jela mchungaji aliyewabaka wasichana wake wawili wa miaka 14 na miaka 16 na kuwapatia mimba
Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi wa Baricho Anthony Mwicigi, alimuhukumumwanaume huyo kifungo cha miaka 70 kwa kila msichana . Mahakama iliamua kuwa hukumu hizo zitatekelezwa moja baada ya nyingine na hivyomchungaji huyo ataishi jela miaka 140.

Mhungaji huyo kutoka kaunti ya Kirinyaga kati kati mwa Kenya, mwenye umri wa miaka 51 alikiri kuwabaka watoto wake tarehe 5 Januari na kuwekwa jela tangu tarehe 7 Januari. Alimlaumu shetani kwa ubakaji huo watoto wake na akawaomba msamaha watoto wake na mahakama.

Hakimu mkazi Anthony Mwicigi alisema kuwa mchungaji huyo alipataikana na hatia kwa kukiri mwenyewe kuwabaka watoto wake na akaagiza hukumu dhidi yake itolewe tarehe 14 Januari.

Mchungaji huyo anayefahamika kwa jina la Gichina alikamatwa mahala alipokuwa amejificha baada ya polisi kuanzisha harakati za kumsaka.

Msichana mmoja tayari ana mtoto wa miezi 7 na mwingine ana mtoto wa miezi 5.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad