Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mwalimu Atuhumiwa Kumtwanga Bakora Mtoto Mpaka Kuzirai

Mwalimu wa shule ya Sekondari Bupandwa iliyoko Halmashauri ya Buchosa Wilaya Sengerema Mkoa wa Mwanza Sara obby anatuhumiwa kumcharaza viboko wanafunzi wa shule hiyo Selefina Augustine (18) anayesoma kidato cha nne hadi kupoteza famahu na kulazwa kituo cha afya mwangika kwa matibabu.

 

 

Tukio hilo limetokea Januari 27 mwaka huu majira ya saa kumi Jioni nyumbani kwa mwalimu huyo baada ya mwanafunzi huyo akiwa na wenzake kumaliza kumutekea maji ya matumizi ya nyumbani mwalimu huyo.

 

 

Selefina Augustine (18) mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondari Bupandwa aliyepokea kichapo toka kwa mwalimu wake na kulazwa kituo cha afya mwangika kwa matibabu alisema yeye wenzeka watano mwalimu huyo aliwaagiza kumteka maji ya matumizi yake ya nyumbani.

 Wakati walipokuwa wakiingiza maji ndani ya nyumba ya mwalimu huyo waliona chakula kikiwa kimeiva aina ya vizia waliamu kuchukuwa Kila mmoja kiazi kimoja kimoja ili wale kutokana na njaa waliyokuwa nayo wakati wakiteka maji ya mwalimu wao.

 

 

Wakati wakiwa katika tendo la kula vianzi hiyo mwalimu huyo alitokea na kuanza kuwafokea huku akiwacharaza viboko kiunoni na mgongoni alipojaribu kukimbia alimshika na kumpigiza chini hadi kupiteza fahamu na hakujua chochote kinachoendelea hadi alipojikuta akiwa amelazwa hospitarini.

 

 

Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wanaosoma kidato cha nne(majina yamehifadhiwa) walisema vitendo vya walimu kuwapiga kisha kuwatumikisha kwenye mashamba yao kutoa adhabu zisizo natija zimekithiri na kuiomba Mamulaka husika iwasaidie.

 

 

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole alisema hana taarifa ya suala hilo ameahidi kulifuatilia na kulipata ufumbuzi. “Sina taarifa tukio hili ngoja nilifuagie nitapata majibu kisha nitachukuwa hatua” alisema Kipole.

 

 

Mama mzazi wa mwanafunzi aliyepokea kichapo toka kwa mwalimu wake Olitha Daudi alisema kuwa walipata taarifa ya mtoto wao kupigwa na mwalimu huyo akiwadaiwa alichukuwa kiazi kimoja kwenye chakula alichokuwa ameendaa kwa ajili ya mchana nyumbani kwake.

 

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa Crispin Luanda alisema amekwisha pata taarifa juu ya tukio hilo na ameahidi kunifanyia kazi.

 

 

Mganga wa kituo cha afya mwangika Dk Fredrick Shoo amekilimpokea mwanafunzi huyo majira ya saa mbili.usiku Jana na kuanza kumpatia matibabu.

 

‘Alisema baada ya Kumpima waligundua anamaumivu kifuani na mgongoni hivyo wanaendelea kumuhudumia ili alejee kwenye Hali yake ya kawaida.” Alisema Shoo.

 

 

Ofisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Buchosa Bruno Sangwa alisema anafahamu suala hilo na wanalifuatilia.Mkuu wa shule akimbia wanahabari

Licha ya kuzungumuza naye kwa njia ya simu na kukili tukio hilo limetokea mkuu huyu Kulwa Mahona aliwakimbia ofisini kwake waandaashi wa habari waliokwenda kweke kutaka kujua chanzo sahihi cha tukiki hilo.

Jitihada za kumpata mwalimu Sara obby kuzungumuza Suala hili halikuweza kupatikana huku watu wakisema huenda ametoka.

 

Wananchi walaani kupewa dhamana aliyemcharaza mwanafunzi bakora.

Baadhi ya wanachi kijiji cha Bupandwa wamelaani kupewa dhamana walimu huyo wakati mwanafunzi huyo akiwa bado anapatiwa matibabu.

 

Kitendo cha mwalimu kumuchalaza bakora wanafunzi wake hadi kupoteza fahamu kimewakela wanachi na kuiomba Serikali ichukue hatua.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments