Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mzee Yusuf Apiga Bonge la Shoo Dar Live, Avunja Kundi la Jahazi
Mfalme wa Taarab Bongo, Mzee Yusuf usiku wa kuamkia leo alipiga bonge la shoo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem Jijini Dar.

Mzee ambaye alikuwa akijulikana kama Mkurugenzi wa Kundi la Jahazi Modern Taarab katika shoo hiyo alitangaza kuliua kundi hilo na kuzindua kundi lake jipya la Safina.

Uzinduzi huo uliongozwa na Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto ambapo baada ya uzinduzi huo Mzee alikitambulisha kikosi chake kipya ambacho atakuwa akipiga nacho kazi. Katika kikosi hicho Mzee amewatambulisha waimbaji pamoja na dada yake Hadija Yusuf, Mishi Zele, Miriam Mwinjuma, Fatma Mahmoud, Mwasity Robert, Fatma Kassim na Laazizi wake Kipenzi, Nyonga mkalia Ini, Mkewe Leyla Rashid.

Baada ya uzinduzi huo jamaa kwa kuonesha amejipanga alianza kupiga nyimbo mpya moja baada ya nyingine na kuwadatisha mashabiki waliofurika kwenye shoo hiyo.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments