Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Rais wa Mexico apata maambukizi ya COVID-19Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez anayefahamika kwa kupuuza kitisho cha janga la virusi vya corona ametangaza kuwa ameambukizwa virusi hivyo usiku wa kuamikia leo.
 Lopez ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba amegundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona lakini anaonesha dalili za kawaida na tayari ameanza kupatiwa matibabu. 

Amesema ana matumaini ya kupata nafuu na ataendelea na shughuli za kila siku za kuongoza taifa ikiwa ni pamoja na mazungumzo ya simu na rais Vladimir Putin wa Urusi yaliyopangwa kufanyika baadae hivi leo. 

Kwa muda mrefu kiongozi huyo ameonesha kutolipa uzito janga la virusi vya corona na mara nyingi huonekana hadharani bila ya kuvaa barakoa.

 Mexico imepoteza zaidi ya watu 149,000 kutoka na ugonjwa wa COVID-19 na kuwa taifa la nne duniani kwa idadi kubwa ya vifo tangu kuzuka kwa janga hilo mwishoni mwa mwaka 2019.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments