Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Wachimba migodi walionasa chini ya ardhi China watuma ujumbe kwa waokoziWachimba migodi walionasa chini ya ardhi mashariki mwa China kwa zaidi ya wiki moja baada ya mlipuko kutokea kwenye mgodi wa dhahabu wamefanikiwa kutuma ujumbe kwa waokozi. 

Mlipuko huo ulitokea siku nane zilizopita Jumapili mchana katika mgodi karibu na mji wa Qixia wa mkoa wa mashariki wa Shandong, na kuwaacha wachimbaji 22 wakiwa wamenasa chini ya ardhi zaidi mita 600 kutoka lango kuu la mgodi huo.


 Baada ya kipindi kirefu bila mawasiliano yoyote, waokozi waliweza kuchimba shimo hadi chini jana mchana na kusema walisikia "sauti za kugonga". 


Ujumbe kisha ulitumwa juu kutoka kwa wachimbaji hao wakisema 12 bado wako hai. Ujumbe huo kwenye karatasi ulisema wanahitaji kwa dharura dawa za ubaridi, kupunguza maumivu, watu watatu wana shinikizo la damu na wanne wamejeruhiwa. 


Desemba mwaka jana, wachimba migodi 23 walifariki baada ya kunasa kwenye mgodi katika mji wa kusini magharibi wa Chongqing -- miezi michache tu baada ya wengine 16 kufariki baada ya kunasa chini ya ardhi katika mgodi wa makaa ya mawe mjini humo.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments