Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Wawili mbaroni kwa wizi wa dawa akiwemo muuguzi

Muuguzi wa zahanati ya Nyamalogo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga William Desdez na Fedson Matekele wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa tuhuma ya wizi wa madawa katika zahanati ya Nyamalogo.


Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba amesema watuhumiwa hao walikamatwa Januari 12 mwaka huu majira ya saa tisa alasiri nyumbani kwa Fedson Matekele ambaye ni sungusungu wa kijiji hicho wakati akiuziwa dawa hizo za binadamu zikiwemo baadhi zimemaliza muda wake.Kamanda Magiligimba amesema watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na dawa hizo baada ya uongozi wa Kijiji cha Mwang'osha kupata taarifa na kuwasiliana na kaimu Mtendaji wa Kijiji hicho pamoja na polisi na kufanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa wote.Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani baada ya taratibu za uchunguzi kukamilika.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments