Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Yanga Kiboko Yatangulia Nusu Fainali..Yampa Kimoko Namungo wa Kimataifa

 


Yanga imetinga nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Namungo FC bao 1-0, mchezo uliochezwa leo Ijumaa usiku kwenye Uwanja wa Amaan kisiwani hapa.


Bao la Yanga lilifungwa na Zawadi Mauya dakika ya 24 baada ya kuliga shuti lililotinga moja kwa moja golini katika mechi iliyokuwa na ushindani mkubwa.


yanga namungoooo

Mechi ya kwanza Yanga walichez ana Jamhuri ya kisiwani Pemba ambapo timu hizo zilitoka sare tasa hivyo mechi ya leo kwa Yanga itatoa mwanga ya wao kusonga mbele kama matokeo yatabaki hivi hivi.


Kwa upande wa Namungo wao ni mechi ya kwanza ambapo baada ya hii watacheza na Jamhuri ili kujua hatma yao kwenye mashindano haya ambayo kilele chake ni Januari 13 mwaka huu.


Timu zote mbili kipindi cha kwanza zilicheza kwa kushambuliana na kukosa nafasi kadhaa za wazi ambapo Namungo dakika ya 33 walikosa mpira ukiwa ni wa piga nikupige langoni mwa wapinzani nao.


Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Namungo walishindwa kusawazisha bao hilo.


Kipindi cha pili makocha wote walifanya mabadiliko ambapo kocha wa Yanga Cedric Kaze alimuingiza Omary Chibada aliyechukuwa nafasi ya Haruna Niyonzima wakati Hemed Morocco kocha wa Namungo naye aliwatoa Shiza Kichuya nafasi ilichukuliwa na Abeid Athman wakati nafasi ya Blaise Bigirimana nafasi yake ilikwenda kwa Sixtus Sabilo.


Morocco alifanya badiliko lingine alimuingiza Idd Kipagwile aliyechukiwa nafasi ya Hassan Manyanya akiwa na lengo la kuongeza mashambulizi baada ya timu yake kuwa nyuma kwa bao 1-0.


Kwa matokeo hayo Yanga wamenusa hatua ya nusu fainali ambapo itazisubiri mechi ya kesho Jumamosi dhidi ya Namungo na Jamhuri ambao walitoka sare na Yanga

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments