Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Afumaniwa Kitandani Akivunja Amri ya Sita na Mke wa Mjeda


NJEMBA mmoja katika Mtaa wa Kawangware, jijini Nairobi nchini Kenya ametokwa na kijasho chembamba baada ya kunaswa akitafuna asali ya wenyewe na kisha kupewa sharti lililomvunja moyo.

 

 

Inasemekana mwenye nyumba ambaye ni Mwanajeshi alimwambia kwa hasira kwamba naye angeenda kwake kulipiza kisasi kwa kuchovya asali ya mrembo wake hadi asubuhi.

 

 

“Kwa kuwa unajiona kidume cha mwanaume kurina asali yangu, ni zamu yangu kwenda kwa mkeo nikakeshe naye. Hautoki humu maana nawafungia kwa kufuli mbili,” alisema Mjeda kwa dharau.

 

 

Kabla ya kijogoo huyo kunaswa, inasemekana alikuwa amemnyemelea mke wa jamaa huyo kwa muda mrefu. “Mzinga wako unarambwa na hauna habari?” jirani alimpasha jamaa.

“Nani anacheza na kifo? Nani huyo asiyethamini maisha yake?” mjeda aliuliza.

“Weka mtego usiku huu na unamjua. Lipo dume linalounguruma kwako pindi ukiondoka,” jirani alijibu.

 

 

Taarifa zaidi zinasema kwamba jamaa alirejea nyumbani usiku huo na kumkuta kidume aliyemfahamu vyema akiwa amempakata mkewe kitandani.

 

 

“Humu ndani mna chakula cha kutosha. Usiwe na haraka kutoka. Leo naenda kuunguruma kwako,” jamaa aliwaka huku akifunga mlango kwa nje. Duru zinasema kwamba kijogoo alishtuka sana na kumuomba jamaa wazungumze.

 

 

“Hakuna cha kuzungumza. Mkuki kwa nguruwe mtamu, kwa binadamu mchungu. Sasa meza ukweli wako hata ingawa unauma!” mjeda aliongea na kuwaacha wawili hao wakikuna vichwa.

 

 

Hata hivyo, haikufahamika iwapo ni kweli jamaa alielekea kwa mke wa njemba huyo, lakini njemba huyo alipooona mambo yamekuwa mabaya alivunja dirisha na kutoroka kuelekea kwake, naye mke wa afande akamfuata akihofia mumewe angemtwanga akirudi.

Chanzo – Tuko News


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments