Mbunge CCM ataka Magufuli kuongezewa muda madarakani

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA

Mbunge wa Makambako (CCM), Deo Sanga leo Jumatano Februari 3, 2021 amerudia kauli yake ya kutaka Rais wa Tanzania, John Magufuli kuongezewa muda wa kukaa madarakani.


Ameeleza hayo bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa hotuba ya Magufuli ya ufunguzi wa Bunge la 12 aliyoitoa mwishoni mwa mwaka 2020.Katika Bunge la 11, Sanga amewahi kueleza jambo hilo zaidi ya mara mbili akitaka kiongozi mkuu huyo wa nchi anayemaliza muda wake wa miaka 10 mwaka 2025, kuongezewa muda ili aendelee kukaa madarakani huku akitaja sababu mbalimbali.Mbali na Sanga, mbunge wa zamani wa Chemba (CCM), Juma Nkamia na aliyekuwa mbunge wa Nkasi Kaskazini kwa tiketi ya chama hicho tawala, Ally Keissy nao waliwahi kuzungumzia suala la Magufuli kuongezewa muda, kauli ambayo iliungwa mkono na Spika Job Ndugai.Hata hivyo Rais Magufuli amekuwa akikaririwa akisema kuwa hawezi kuongeza muda. Machi mwaka 2020 katika mahojiano maalum na Mwananchi katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally alisema  Magufuli hana mpango wa kubadilisha Katiba ili kuendelea kukaa madarakani kwa awamu ya tatu na wanaosema hilo watafute mtu mwingine wa kufanya hayo."Huyu Magufuli (John) lazima aongezewe muda, atake asitake tumuongezee mbona mataifa mengine kama China walifanya hivyo," amesema Sanga bungeni leo.


Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
 1. SWADAKTA, SISI WANANCHI TUNATAKA HILI JEMBE ADIMU, LIENDELEE KUTUTUMIKIA.

  KINA MAGUFULI HAWAPATIKANI MARA KWA MARA.

  MCHAMUNGU, MZALENDO, MUADILIFU, MCHAPA KAZI, MTETEZI WA WANYONGE NA MBUNIFU. MSIKIVU KUBWA ZAIDI NI GAME CHANGER IN AFRICAN LEADERSHHIP.

  IKIWA URUSI NA UCHINA WAMEWEZA. SISI TUSHINDWE NINI..??

  MAGU BABA,KILIO NA OMBI LETU TUNAKKUOMBA UKUBALI TUKUONGEZEE MUDA MPK 2035

  ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad