Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Ronaldo Fundi wa Soka Anayezeeka na Makali yake

 


Mshambuliaji nyota wa klabu ya soka ya Juventus Cristiano Ronaldo, leo 5/2/2021 anatimiza miaka 36 tangu kuzaliwa kwake.


Ronaldo aliyezaliwa 5/2/1985 mji wa Madeira Ureno, amekuwa moja ya wachezaji wenye mafanikio makubwa sana  katika historia ya mchezo wa soka Duniani, tangu alivyoanza rasmi soka la ushindani katika klabu ya Sporting CP ya nyumbani kwao mwaka 2003.


Alianza kufanikiwa kimataifa zaidi alivyojiunga na Manchester United  mwaka  huo huo  2003 na kudumu kwa miaka 6. Alifanikiwa kufanya makubwa, kwa  kutwaa vikombe mbalimbali vya ligi za ndani pia kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa  Ulaya 'UEFA' mwaka 2008, pia alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa  Dunia ''Ballon d'or''.


Ronaldo alihamia  klabu ya Real Madrid mwaka 2009 na kutambulisha 'ufalme' wake, kwa kufanya vizuri kama timu na yeye binafsi  alifanikiwa zaidi kutwaa vikombe mbalimbali hasa kwenye ligi ya mabingwa wa Ulaya mara 4 katika uwepo wake Madrid kwa miaka takribani 10 ambapo ilikuwa mwaka 2013-14, 2015-16,2016-17  na 2017-18.


Mwaka 2018, Ronaldo alihamia klabu ya Juventus kwa uhamisho ulioshtua Dunia, wengi wakimtaja  kuwa mzee na amekwisha kiuchezaji kutokana na umri wa miaka  33 aliyokuwa nayo , lakini huko nako alipata mafanikio ya kutosha ikiwemo ubingwa  mara mbili mfululizo wa ligi ya Italy.


Cristiano  Ronaldo anatimiza miaka  36 leo, umri ambao kisoka tunasema ni mzee lakini kwake imekuwa tofauti sana, kama uwezo unaongezeka kila kukicha, kwa sasa anaongoza kwa magoli katika ligi ya Italy akiwa amefunga magoli 15 katika mechi 16 akiwa amecheza jumla ya dakika 1,374 tu.


Ronaldo pia  amefikia na kuvunja rekodi ya ya mfungaji bora wa muda wote wa magoli kwa mechi rasmi akiwa amefunga magoli 763 na kumpita  Joseph Bican, mshambuliaji wa zamani wa Urusi aliyefunga magoli 762, amefanya haya akiwa anakaribia kutimiza miaka hiyo 36.

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE

Takwimu za Ronaldo zinaonesha ameifungia Sporting CP magoli 5 katika michezo 31, Manchester United magoli 118 katika michezo 292, Real Madrid magoli 450 katika michezo 438 na Juventus magoli 87 katika michezo 112, pia ameweza kumudu kufunga magoli zaidi ya 300 akiwa amefikisha umri wa miaka 30.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments