Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Country Boy afunguka ukimya wa Cheed na Killy

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Rapa Country Wizzy kutoka lebo ya Konde Gang ya Harmonize amefunguka ukimya wa wasanii Killy na Cheed ambao tangu wamehamia kwenye lebo hiyo wakitokea Kings Music ya Alikiba wamekuwa kimya kwenye kuachia kazi.

 

Akizungumzia suala hilo ambalo mashabiki wengi wamekuwa wakihoji juu ya ukimya wao kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi wakidai wamefulia Country Wizzy amesema 


"Ukimya wa Killy na Cheed ni unasababishwa na ubize wa kutengeneza Album, ambapo walipanga watoke na style hiyo na wapo katika hatua ya mwisho kukamilisha Album yao na kabla ya mwezi wa tano itakuwa tayari, Killy ana ngoma moja kali sana kwenye Album yake  ninayo kwenye simu yangu".


Aidha tangu alivyosainiwa Konde Gang rapa Country Wizzy tayari ameshaachia EP moja, kupewa zawadi ya gari na sasa hivi anatamba na ngoma yake mpya ya 'Baby'

Post a Comment

0 Comments