Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Uganda kuomboleza siku 14 kifo cha Magufuli

 


Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema nchi yake inaungana na Watanzania kuomboleza kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kutangaza siku 14 za maombolezo ambapo bendera zote zitapepea nusu mlingoti.

 

Rais Museveni ameandika hayo katika ukurusa wake wa Twitter na kutoa pole kwa Watanzania kufuatia msiba huo mzito huku akimpongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Akimuelezea Hayati Dkt. Magufuli amesema alikuwa ni rafiki wa ukweli kwa Uganda, bingwa wa kujitoa katika upatanishi wa uchumi wa Afrika Mashariki na maendeleo, mwenye msimamo wa wazi wenye kutia nguvu katika masuala ya Tanzania na Afrika.


Sambamba na hayo Rais Museveni amesema nchi ya Tanzania itaukumbuka uongozi wake uliotukuka  na mchango wake ambao walikuwa wanautengea kwa muhula wake wa mwisho katika nafasi yake ya uongozi.

 

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments