Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

"Vanessa Mdee arudi bongo kuna nini" - Mimi Mars

 


Vanessa Mdee arudi bongo kuna nini, hilo ni jibu ambalo amelitoa msanii Mimi Mars baada ya kuulizwa kuhusiana na dada yake Vanessa Mdee ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani na mpenzi wake Rotimi.

 

Akipiga stori na Big Chawa kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio Mimi Mars amesema anam-miss dada yake Vanessa Mdee japo wanawasiliana kila siku kwa njia ya kupigiana simu na message.


"Arudi wapi "Bongo" kuna nini, tunamisiana sana lakini tunaongea kila siku kwa kupigiana simu na kutumiana message wala hatuna tabu hata kama yupo kule lakini bado yeye Mdee Music na anaendelea kusimamia harakati na michongo ya kwangu na ananishauri vitu mbalimbali ili tuzidi kutoboa" ameeleza Mimi Mars


Vanessa Mdee anaishi nchini Marekani baada ya kuanzisha mahusiano na msanii wa filamu na muziki nchini Marekani ambaye ana asili ya Taifa la Nigeria Rotimi ambapo kabla ya hapo alikuwa na Juma Jux.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments