Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Waziri mkuu awatuliza Watanzania "Rais Magufuli aumwi yupo salama, kutoka kwake ni kwa ratiba"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka Watanzania kuwapuuza wapotoshaji wanaosambaza taarifa za chuki, uongo na kuzua taharuki miongoni mwa wanajamii kuhusu afya ya Rais Dkt. John Magufuli na kusema kuwa ni mzima wa afya na hata leo asubuhi ameongea naye.
Akizungumza baada ya Swala ya Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa mkoa wa Njombe, Waziri Mkuu amesisitiza kumekuwa na tabia ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi ya kupotosha kwa makusudi mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi pamoja na kuzusha uongo.

"Kwa hili na mimi nioneshe masikitiko yangu kwa wanaosambaza uzushi juu ya afya ya kiongozi wetu na kuleta taharuki kuwa Rais wetu anaumwa jambo ambalo ni uongo kwani mimi asubuhi nilizungumza naye nikamfahamisha juu ya ziara yangu mkoani Ruvuma," Aliongeza Waziri Mkuu Majaliwa

"Rais ana mambo mengi na kutoka kwake ni kwa ratiba ya mpango kazi wake, unataka Rais atoke aanze kuzurura Kariakoo au aanze kuzurura Magomeni au unataka azunguke kwa ratiba yako?" ameongeza Majaliwa.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa, amewataka Watanzania kuwaombea viongozi wakuu wa nchi kwani wana dhamana kubwa ambayo wamepewa na Watanzania ya kuwatumikia

Post a Comment

0 Comments