Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Zari Atoa Pole Kwa Watanzania Kuondokewa JPM

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
MAPENZI yanaweza kufika ukingoni, lakini uhusiano ukadumu milele!Hicho ndicho kinachotokea kwa mwanamama mwenye pesa zake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady ’ kwani kuna kila ishara kwamba, bado ana mawasiliano mazuri na mzazi mwenzake ambaye ni staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Planumz’.

 

Zari ambaye amezaa watoto wawili na Diamond au Mondi ametoa pole kwa Watanzania kwa kuondokewa na Rais wao kipenzi, Dk John Pombe Magufuli aliyeaga dunia, juzi jijini Dar.

 

Juzi, Zari ambaye ni raia wa nchini Uganda mwenye maskani yake Durban, Afrika Kusini, alitumia ukurasa wake wa Instagram kutoa pole kwa msiba huo mzito kisha kuonesha ishara ya kuolewa Bongo baada ya kueleza uhusiano wake na Wabongo ambao ni mashemeji na mawifi zake kwa Mondi.Zari amefumbua fumbo la muda mrefu kwamba, huwenda alifunga ndoa na Mondi ndiyo maana akatoa pole kwa Rais Magufuli akimtaja kama baba mkwe wake.

 

“Lala salama baba mkwe,” ameandika Zari.Utambulisho huo wa kumuita Rais Magufuli baba mkwe wangu, umeibua mjadala mzito kwa kuwa inafahamika uhusiano wake na Mondi ulifikia ukingoni siku ile ya Februari 14, 2018.

 

Februari, mwaka huu, Zari alimuonesha kwa mara ya kwanza mwanaume wake wa sasa ikiwa ni ishara kwamba hana mpango tena na Mondi.

 

Hata hivyo, kitendo cha kumlilia Rais Magufuli kwa kumuita baba mkwe ni ishara kwamba bado kuna kitu kinaendelea kati yake na Mondi.

 

Zari anaungana na Mondi na mastaa kedekede wa ndani na nje ya Bongo ambao wameendelea kumlilia Rais Magufuli ambaye alifariki dunia, juzi kwa maradhi ya moyo.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments