Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Matola, Bocco watamba mechi ya kesho dhidi ya AS Vita

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Kocha msaidizi wa klabu ya Simba, Selemani Matola amesema siku ya kesho ya tarehe 3 April 2021 ni  lazima wapate matokeo watakaposhuka kwenye dimba la mkapa saa 10:00 jioni kupepetuana na klabu ya AS Vita ya Jamhuri ya DR Congo kwenye mchezo wa mzunguko wa tano wa klabu bingwa Afrika.
Akiongea mchana wa leo mbele ya wanahabri, Matola amesema “Kesho ni lazima tupate matokeo ili tusonge mbele, tumejipanga kupata matokeo. Tunamshukuru Mungu hakuna mchezaji ambaye tutamkosa, wote wapo kambini na hilo linatupa mwanga kuwa tunaweza kufanya vizuri”.

Nae Nahodha wa klabu ya Simba John Bocco amesema wao kama wachezaji wapo vizuri kwani watafanya kila ambalo linawezekana na yale yote ambayo mwalimu amewaelekeza ili kuhakikisha wanaondoka na ushindi kwenye mechi hiyo.

“Kwa upande wetu kama wachezaji tuko vizuri, tuna ari nzuri ya kuweza kupambana ili kufikia malengo ya timu yetu. Tumefanya maandalizi mazuri na tunaamini Mungu atatusaidia na tutafuzu hatua ya robo fainali”.

“Tuna wachezaji wenye uzoefu mkubwa na wanaoelewa kwanini wapo kwenye klabu. Tuko tayari”. Akamalizia, Bocco.

Ikumbukwa kuwa Simba ni kinara wa kundi A akiwa na alam 10 huku akihitaji alama 1 kutinga hatua ya robo fainali, Al Ahly ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 7, AS Vita ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 4 na endapo watapoteza mchezo huo watashindwa kusonga mbele sawa na Al Merrick mwenye alama 1.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments