Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Misri yagundua mji uliokuepo miaka 3,000 iliyopita


Wataalamu wa historia ya nchini Misri wamefanya ugunduzi wa kushangaza wa mji ambao ulikuepo zaidi ya miaka 3,400 wakati wa muda wa farao.
Uzinduzi huo umetajwa kuwa muhimu tangu kugunduliwa kwa kaburi la kale la Tutankhamun.

Wana akiolojia hao ambao walikuwa wakitafuta hekalu katika eneo la jangwa karibu na mji wa Luxor. Lakini wakaanza kugundua jambo lingine, ukuta wa nyumba ambazo zilionekana kila upande.

Kulikuwa na vyumba vilivyokuwa na vitu ambavyo Wamisri wa kale walikuwa wakitumia kila siku atika maisha yao.

Pete na vyungu vilivyochorwa kwa rangi na kugongewa muhuri wa farao aliyekuwa na nguvu kubwa nchini humo .

Kulikuwa na duka la kuuza mikate katika eneo la jirani ambapo ushahidi wa maandalizi ya chakula cha watu wengi yalionekana.

Sehemu nyingine kulikuwa na ishara ya shughuli za kiwanda.

Inaonekana kuwa wakazi wa eneo hilo walikuwa wanajishughulisha kutengeneza mapambo ya maeneo ya kuzikia na hekaluni.

Uzinduzi huo ulikuwa na taarifa nyingi hata kuhusu majibu ya kwanini eneo hilo lilitelekezwa na watu wake.

Ugunduzi huu ni jambo muhimu sana katika historia ya Misri na wataalamu wake wa akiolojia.

Mji huu uliohifadhiwa vizuri umeelezewa kuwa kumbukumbu ya historia ya Misri.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments