Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Muro Anasa Vijana Wawili Mtandao Wa Wizi Mifugo

MTANDAO wa wizi wa mifugo umenaswa wilayani Arumeru baada ya vijana wawili ambao wanatajwa kuongoza mtandao huo kutiwa mbaroni.


Vijana hao wanadaiwa kuongoza uvunjaji wa mabanda na mazizi ya wananchi na kisha kuiba ng'ombe  na mbuzi na  kuchinja usiku ambapo alfajiri hupeleka nyama mabuchani.Mtandao huo umenaswa baada ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro kufanikiwa kuwadaka vijana hao wakiwa na pikipiki mbili wakitupa ngozi pamoja na kitoto kichanga cha ng'ombe kilichofia tumboni baada ya kuchuna ngozi.Alisema ameamua kuendesha msako huo baada ya kuibuka malalamiko kutoka kwa wafugaji waliodai mifugo yao kuvamiwa nyakati za usiku na kwenda kusikojulikana.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments