Sanchi Afunguka Baada ya Kuanza Maisha Mapya

MREMBO mwenye figa matata Bongo, Janey Rimoy ‘Sanchi’ amesema hajutii kutofuta picha zake za zamani ambazo zilikuwa zikimuonyesha nusu utupu kwa sababu anaamini zaidi mahali alipo kwa sasa na sio alikotoka.

 

Akizungumza na AMANI mwanadada huyo ambaye miezi michache iliyopita alibadili dini kutoma ukristo na kuwa muislamu kisha akapewa jina la Surraiya, alisema kuwa baada ya kuamua kuachana na mambo ya kidunia na kumrudia Allah baadhi ya watu wamekuwa wakimuuliza kuwa kwanini hajafuta picha zake za zamani.

 

Alisema maswali hayo kwake si jambo la msingi kwani anazingatia zaidi imani aliyonayo kwa Mungu wake.“Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiniuliza kwanini sijafuta picha zangu za zamani kwenye akaunti yangu ya Instagram, ukweli ni kwamba nilifuta picha zote labda zilizobaki ni chache sana.

 

‘Lakini hiyo hainisumbui kwa sababu sijutii kitu chochote, na pia bado nataka kuwaonyesha watu kuwa inawezekana kabisa mtu akabadilika na kuwa mtu mwingine, lakini pia naangalia zaidi hapa nilipo na sio nilikotoka,” alisema Sanchi.

STORI; KHADIJA BAKARI NA MEMORISE RICHARDđŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad