Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Watu 26 wafa baada ya boti kuzama Bangladesh

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
Watu 26 wamekufa baada ya boti waliyokuwamo, kugongana na meli ya mizigo na kuzama kwenye mto mmoja ulio karibu na mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka. Waokowaji waliikuta miili 21 ndani ya boti hiyo, huku miili mingine mitano ikiopolewa masaa kadhaa baada ya ajali hiyo iliyotokea jana. 


Kwa mujibu wa mkuu wa mamlaka ya usafiri wa majini ya nchi hiyo, Kamadoo Ghulam Sadiq, boti hiyo ilikuwa imebeba abiria 50 wakati inapata ajali. Picha za video zilizorushwa moja kwa moja zilionesha waokowaji wakiopowa miili kutoka kwenye boti hiyo wakati ikipelekwa kwenye kingo za Mto Shitalakshya. Kwa mujibu wa Kamadoo Ghulam Sadiq, abiria wengine walijiokowa wenyewe kwa kuogelea hadi kwenye fukwe za mto huo, ingawa bado wanaendelea na msako.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments