CCM kumpeleka Zitto mahakamani ikidai kudhalilishwaBaada ya kiongozi ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kudai kuvamiwa na gari tatu za CCM, Katibu wa chama hicho tawala Mkoa wa Kigoma, Kajoro Vyohoroka amesema wanasubiria matokeo yatangazwe wafungue jalada mahakamani la kudhalilishwa na kiongozi huyo.


"Sisi kwenye kampeni tulikuwa na magari 48 katika Jimbo la Muhambwe pekee sawa na gari mbili kila kata sasa yeye kaona magari yanapita kwenye vituo huko akaanza kusambaza taarifa yanasambaza kura bandia tutamchukulia hatua baada ya matokeo kutangazwa," amesema Vyohoroka.Mwenyekiti huyo wa ACT Wazalendo alituma ujumbe mfupi kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter uliosomeka," tumetoka polisi. OCD wa Kibondo ametusaidia sana. Tupo salama. Tunaendelea kulinda ushindi wetu hapa Muhambwe mpaka mwisho. Polisi wamefanya kazi kwa weledi kabisa. Ni hatua kubwa.”Awali, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama alisema tuhuma hizo sio za kweli huku akiwahakikishia wakazi wa jimbo hilo kwamba jeshi hilo halijapokea taarifa yoyote ya uwepo wa kura bandia.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE