.

5/27/2021

Dawa hizi zinaweza kusababisha ini, figo 'kufeli'MATUMIZI ya muda mrefu ya dawa tiba zenye asili ya kulevya kama Pethidine, Valium, Morphine, Tramadol na nyingine nyingi zimetajwa kuwa chanzo cha ugonjwa wa ini na figo.

Hayo yamesemwa leo Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk Peter Mfisi katika kikao kazi na baadhi ya waandishi wa habari, kilichofanyika ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Mfisi alisema athari za matumizi ya dawa hizo zinamlenga mtumiaji moja kwa moja na jamii kwa ujumla.

Alisema matumizi holela ya dawa hizo kwa muda mrefu au kwa kutumia dozi kubwa uleta madhara makubwa katika miili yao ikiwepo magonjwa ya figo, ini, pamoja na uraibu wa dawa hizo.


 
“Dawa hizi hutumika hospitali kwa matibabu ya magonjwa mbalimbali, lakini waraibu wa dawa za kulevya pia wanapokosa  dawa za kulevya wanageukia dawa hizi kama mbadala wa dawa za kulevya kwa sababu inaaminika kuwa dawa hizi zinapotumika kinyume na ushauri wa madaktari zinaweza kuleta matokea sawa na dawa za kulevya.” alisema

Alisema watu wanaotumia dawa tiba zenye asili ya kulevya hulazimika kubadili dozi ya kawaida inayotolewa na daktari na kuifanya ya juu zaidi akitolea mfano dawa aina ya tramadol inayotumika kutibu maumivu,  dozi yake ni kati 50mg hadi 100mg ambapo mgonjwa atatumia kati ya mara moja au mbili kwa siku na kwa  muda maalumu.

“Ila sasa watumiaji wa dawa hizo kwa kujifurahisha wanaweza wakatumia kati ya 500mg hadi 1000mg kwa siku na matumizi haya yanachukua muda mrefu zaidi,”alisema


Dk Mfisi alisema matumizi ya dozi kubwa kwa muda mrefu huweza kuleta madhara makubwa katika miili yao ikiwepo magonjwa ya figo, ini, pamoja na uraibu wa dawa hizo.

Alisema baada ya udhibiti wa Dawa za Kulevya kuwa mkubwa upatikaji wa dawa hizo umekuwa mgumu, zinapatikana kwa uchache na kwa kificho.

“Hali hiyo imesababisha watumiaji wa dawa hizo kugeukia kwenye matumizi ya dawa tiba zenye asili ya kulevya kama vile Pethidine, Valium, Morphine na Tramadol na nyingine nyingi.

Alisema dawa hizo  hutumika hospitali kwa matibabu ya magonjwa mbalimbali, lakini waraibu wa dawa za kulevya wanapokosa kosa dawa za kulevya wanageukia dawa hizi kama mbadala wa dawa za kulevya kwasababu inaaminika kuwa dawa hizi zinapotumika kinyume na ushauri wa madaktari zinaweza kuleta matokea sawa na dawa za kulevya.

 “Dawa hizi zinawafikia watu kutokana na baadhi ya wahudumu wa afya wenye dhamana ya kutunza dawa  kuzitoa kiholela.

Aidha amedai dawa hizo zimekuwa ikiuzwa kwenye maduka ya dawa bila kuwepo na cheti cha daktari kama inavyotakiwa hivyo kusababisha dawa hizo kuwafikia waraibu kwa ukaribu, Pia baadhi ya wafanya biashara wamekuwa wakiziingiza nchini bila kibali maalumu”.

Alisema katika kutatua changamoto hii, Mamlaka ya udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na bohari ya dawa , bodi ya famasia, Mamlaka ya dawa na vifaa tiba pamoja na maabala ya mkemia mkuu wa serikal wamefanya mawasiliano kuongeza udhibiti wa dawa hizi ili zisipatikane kiholela
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger