Kumbe Sanchi Hakubadili Dini Sababu ya Mwanaume
MREMBO mwenye figa matata Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’ ambaye kwa sasa anaitwa Surraiya baada ya kubadili dini ya kikristo na kuwa muislamu, amekanusha tetesi za yeye kubadili dini kwa sababu ya mwanaume.

Akizungumza na MIKITO NUSUNUSU, mwanadada huyo alisema kuwa watu wengi wanasema aliamua kuingia kwenye dini ya kiislamu ili aolewe wakati sio kweli kwani aliamua kufanya hivyo kwa sababu yeye mwenyewe alipenda.

“Mimi sijaolewa na wala sikubadili dini ili niolewe, bali niliamua kufanya hivi kwa sababu napenda dini ya kiislamu lakini pia nilitaka kuachana na mambo ya kidunia ili mwisho wa siku nije kuwa mfano hata kwa watu wengine wanaonifuatilia na sio vinginevyo,”

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

1 [disqus]:

  1. OVYOOO kwani kwenye ukristo huwezi kuachana na mambo ya dunia??

    ReplyDelete