Majibu ya Billnass kuhusu kumtumia mwanafunzi

 


Ukiitazama video ya tatizo ya Billnass utamuona 'Video Queen' ambaye ni msanii wa filamu na mwanafunzi Jenipher Kanumba ambapo kwa mara ya kwanza amefanya kazi tofauti na ile watu waliyozoea.

 

Sasa Billnass amesema aliamua kumtumia Jenipher Kanumba kama video queen kwa sababu ya kuleta mazingira kama ya kwenye filamu pia alifuata taratibu zote kwa sababu bado ni mwanafunzi wa chuo.


"Tulitaka mtu ambaye anaweza kufanya kwenye mazingira ya filamu zaidi, tukaona anastahili na tukafuata taratibu zote za kumpata kwa kushirikisha familia yake ili kuhakikisha kwamba analifanya kwa ustadi wa hali ya juu, ni kweli bado mwanafunzi lakini wa chuo ndio maana ile video haja-act kama vixen au ya ku-party ila amecheza kama muigizaji" amesema Billnass 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE